Hassan Moyo afutwa chama,Zanzibar

Image caption Mzee Hassan Nassor Moyo afukuzwa CCM

Mwenyekiti wa Kamati ya Maridhiano ya Zanzibar, Mzee Hassan Nassor Moyo amevuliwa uanachama wa chama cha mapinduzi CCM, hatua iliyofijkiwa na Halmashauri Kuu ya CCM ya Mkoa wa Magharibi, Unguja viswani Zanzibar jana jioni. Mzee Hassan Nassor Moyo anafutiwa uanachama wake ndiye Mratibu Mkuu wa Maridhiano ya Zanzibar ya Novemba 5, 2009 yaliyowakutanisha Rais Mstaafu wa Zanzibar (awamu ya sita), Dk Aman Abeid Karume na Maaalim Seif Sharif Hamad katika kutafuta mbinu ya kuondoa tofauti iliyokuwepo. Maridhiano hayo yameleta faraja kubwa kwa wananchi wa Zanzibar, hasa katika kipindi cha kuelekea Uchaguzi Mkuu uliyopita wa mwaka 2010. Mzee Moyo kwa muda mrefu anadaiwa kuungana na asilimia kubwa ya wananchi wa Zanzibar, wanataka kuiona Zanzibar ikiendesha shughuli zake za kiutawala na kiuchumi bila kuingiliwa na mambo ya Muungano. Hata hivyo kufuatia Mzee moyo, kutuhumiwa kuwa alishiriki katika mapinduzi ya Zanzibar ya Januari 12, 1964 na kusababisha mauaji ya watu 14,amekuwa akikanusha waziwazi madai hayo. Mzee Moyo alikuwa mwanachama wa Chama cha Afro Shirazi (ASP) tangu kilipoanzishwa Februari 5, 1957 baadaye Februari 5, 1977 akajiunga na chama cha Mapinduzi akiwa na kadi namba 7. Kauli za kutisha zinazoashiria kuwa Tanganyika ni Mkoloni mpya kwa visiwa vya Unguja na Pemba, ni pamoja na kauli ya Mizengo Pinda kuwa Zanzibar si nchi, na kauli za hivi karibuni za Samuel Sitta na William Lukuvi. Kauli zinaonekana kuwa mwiba miongoni mwa Wazanzibari. Wahenga walisema: “Ukidharau Mwiba Utakatwa Mguu” Maana yake ni kwamba iwapo bado kuna Wazanzibari hadi sasa wanazipuuza kauli za viongozi hawa wa Tanganyika, wasubiri kukatwa mguu. Mzee Moyo, hayuko tayari kuwa dalali wa nchi yake. Hao wanaosubiri ushahidi kamili wapaswa kutambua kuna siku watakuja kujuta. Mzee Hassan Nassor Moyo, kaona mbali.