Houthi kuendeleza mapigano,Yemen

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Wapiganaji wa Houthi,Yemen

Kiongozi wa waasi wa Houthi nchini Yemen wameituhumu Saudi Arabia kwa mdaia kuwa inajaribu kuwavamia kwa lengo la kutawala nchi yao.

Akizungumza kwa njia ya Televisheni , Abdel Malek al-Houthi amesmea watu wake wana haki ya kujilinda kwa namna yoyote dhidi ya uvamizi huo. Saudi Arabia ikiongoza majeshi ya pamoja kwa ipo katika wiki ya nne ikiongoza mashambulizi dhidi ya waasi hao ili kuhakikisha hawajitanui na kutawala maeneo yote ya Yemen. Mamia ya watu wamekufa kutokana na mabomu na mapigano yanayoendelea kati ya wapiganaji wa Houthi na majeshi yanayomuunga mkono Rais wa Yemen Abd Rabbuh Mansour Hadi.