Wahamiaji 20 zaidi wazama Mediterenian

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Wahamiaji waliokolewa Mediterenian

Kwa mujibu wa msemaji wa shirika hilo la IOM watu ishirini wameripotiwa kufariki.

Aliyetoa ujumbe huo wa dharura amesema, boti tatu zinahitaji misaada katika eneo la kimataifa la bahari hiyo.

Mawaziri wa muungano wa Ulaya, EU, wanakutano mjini Luxembourg, leo kujadili mzozo huo wa uhamiaji baada ya mamia ya watu kuzama mwishoni mwa juma lililopita, baada ya boti yao kuzama katika pwani ya Libya.

Afisa mkuu anayehusika na masuala ya nchi za kigeni wa EU, Federica Mogherini, amesema kuwa mataifa ya bara Ulaya yanapaswa kushughulikia tatizo hilo la wahamiaji katika bahari ya Mediterranean.

"Tunawajibika kisiasa na kwa misingi ya kibinadam kutekeleza majukumu yetu. Bahari ya mediterenian ni letu na ni sharti tuchukuE hatua kama raia wa Ulaya. Ni kwa manufaa yetu, hadhi ya muungano wa ulaya na dhamira kuu ya kuundwa kwa muunganoi huu ni kulinda haki za kibinadam, heshima ya binadamu na masiha ya watu, ni lazima tuzingatie hayo'' Alisema Mogherini.

Baadhi ya mataifa ya Kusini mwa Ulaya yanasema kuwa hadhi ya EU, imehujumiwa kufuatia uamuzi wake wa mwaka uliopita wa kupunguza shughuli za uokozi.

Umoja wa Mataifa umesema njia ya kutoka Kaskazini mwa Afrika hadi Italia na Malta imegeuka na kuwa hatari zaidi duniani.