Andrew Cuomo aitembelea Cuba

Haki miliki ya picha EPA
Image caption Andrea Cuomo

Andrew Cuomo amekuwa gavana wa kwanza kuzuru Cuba baada ya zaidi ya miaka 50 ziara kama hiyo kufanyika.

Cuomo aliongozana na msafara wa wafanyabiashara kutoka New York hadi kwenye kisiwa ambacho mazungumzo hayo yalipangwa kufanyika na Waziri wa biashara wa Cuba..

Akizungumza mjini Havana Cuomo amesema kuwa kutengwa kwa Cuba ambayo ndiyo sera ilidumu miaka mingi haijasaidia.

Mahusiano kati ya Havana na Washington yalianza kuimarika tangu mwezi desemba mwakajana,pale Rais Barack Obama alipomtembelea Rais mwenzake, Raul Castro, na kutangaza nia ya kurejesha mahusiano ya kawaida bila vikwazo.

Hata hivyo mapema mwezi huu mjini Panama rais Obama nan a mwenyeji wake wa Cuba suala la kuondolewa vikwazo dhidi ya Cuba lilibainishwa wazi.