Raia wachoma magari ya hospitali ,India

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Polisi wa India akituliza ghasia

Makundi ya raia wenye hasira kutoka vijiji vya Mashariki mwa wamevamia hospitali ya serikali na kuchoma moto magari kutokana na hasira baada ya kubaini kuwa madaktari hawakuwepo kituoni hapo.

Raia hao wenye hasira walifika hospitalini hapo kuwapeleka kundi la wanafunzi walijeruhiwa vibaya kutokana na ajali za barabarani ambapo baada ya kuwakosa wahudumu wa hospitali hiyo wakaanza kufanya uharibifu huo. Chanzo cha ajali hiyo ambayo ilisababisha wanafunzi kadhaa kujeruhiwa ilitokea baada ya gari moja kugonga gari ya wanafunzi hao ilikuwa imeegeshwa na hivyo kusababisha vifo vya wanafunzi sita katika wilaya ya Siwan jimbo la Bihar nchini India. Polisi wa kutuliza ghasia walilazimika kutumia nguvu ili kuweza kuwatawanya wananchi hao eneo hilo la afya.