Wafuasi wa dhehebu wauawa Angola

Image caption Ramani ya Angola

Wanachama kadha wa dhebu moja lililojihami wameuawa kwenye mapigano na vikosi vya usalama nchini Angola.

Chama kikuu cha upinzani nchini humo cha UNITA kilisema kuwa huenda watu 200 waliuawa huku chama tawala cha MPLA kikisema kuwa ni watu 13 waliuawa.

UNITA kinaitaka serikali ya Angola kuchunguza vifo vya waumini wa dhebu la Seventh Day Light of the World ambalo lilijitenga kutoka kanisa la Seventh Day Adventist.

Dhehebu hilo linamini kuwa dunia itaisha mwishoni mwa mwaka huu na limetoa witu kwa wafuasi wake kuondoka makwao na kuelekea milimani.