Mapigano mapya Malakal, Sudan Kusini

Haki miliki ya picha AP
Image caption wapiganaji nchini Sudan Kusini

Mapigano yameshuhudiwa kwenye mji wenye utajiri wa mafuta wa Malakal nchini Sudan Kusini kati ya jeshi la serikali na kundi hasimu linaloiunga mkono serikali.

Mapigano hayo yalianza siku ya Jumanne usiku ndani ya makao ya gavana. Watu kadha wamejeruhiwa na takriba watu 2000 wamekimbilia usalama kwenye kambi ya Umoja wa Mataifa.

Mji wa Malakal ulio kaskazini mashariki mwa jimbo la Upper Nile umeripoti mapigano ya mara kwa mara tangu kuanza kwa vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini Sudan Kusini mwaka 2013.

Mji huo umedhibitiwa nyakati tofaui na waasi pamoja na vikosi vya serikali.