Tumehitimisha mashambulizi:Saudi Arabia

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption mashambulizi ya anga nchini Yemen

Saudi Arabia imesema imehitimisha Kampeni za mashambulizi dhidi ya Waasi wa kihuthi nchini Yemen.

Wizara ya ulinzi ya Saudi Arabia imesema sasa nguvu itapelekwa kutafuta suluhu ya kisiasa na kuzuia mashambulizi ya wapiganaji wa kihuthi.

Lakini wamesema Vikosi vya kijeshi vitatumika tu ikiwa vitahitajika, na operesheni zinaweza kuendelea kwa kiasi.

Iran ambayo inawaunga mkono waasi, imeelezea kauli ya Saudi Arabia kuwa ya kupiga hatua.

Nae Msemaji wa ikulu ya Marekani, Josh Earnest,amesema Marekani imezitaka pande zote mbili zilizo kwenye mgogoro nchini Yemen, kufanya mazungumzo ili kupata suluhu.

Baada ya kampeni za mashambulizi ya mwezi mmoja zilizotekelezwa na Sudi Arabia, Serikali ya Yemen bado haijarejeshwa.Kadhalika wanamgambo wa kihuthi bado wanadhibiti mjini mkuu, Sanaa.