Libya:Waasi wanawazuia wahamiaji 400

Haki miliki ya picha AP
Image caption Wahamiaji wanaoelekea Italy

Mkuu wa utawala wa waasi nchini Libya ameiambia BBC kuwa vikosi vyao vinafanya juhudi ziwezekanazo kuzuia wahamiaji haramu kuabiri meli kuelekea Ulaya .

Khalifa Al-Ghwell - ambaye serikali yake ya uokozi yenye makao yake mjini Tripoli haitambuliwi kimataifa anasema walinzi wa Libya wa mwambao wamekuwa wakiwashikilia karibu wahamiaji mia nne - kutoka nchi za Sahara barani Afrika katika kipindi cha siku chache zilizopita .

Bwana Ghwell amesema kuwa wahamiaji elfu 17 walikuwa wanaishi katika kambi ya hifadhi nchini Libya , lakini ni asilimia karibu tano walioweza kuvuka na kuingia Ulaya.