Obama:Mateka waliuawa kwa bahati mbaya

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Warren Weinstein

Ikulu ya Marekani imetangaza kuwa watu wawili waliokuwa wamezuiliwa na wapiganaji katika nyumba moja nchini Afghanistan, waliuwawa kimakosa na majeshi ya Marekani yanayopambana na ugaidi katika maeneo ya Afghanistan na Pakistan.

Akisoma taarifa kuhusiana na vifo hivyo, Rais Barrack Obama, amesema kuwa amesikitishwa mno na kisa hicho kilichofanyika Januari mwaka huu.

Anasema watu hao walikuwa wamezuiliwa na wapiganaji wa al Qaeda, kwa miaka kadha.

Wametajwa kama Mmarekani Warren Weinstein, na Giovanni Lo Porto raia wa Italia.

White House inasema pia kuwa, raia wengine wawili waliouliwa walikuwa waamerika, na wanachama wa kundi la al Qaeda.