Rai Jakaya Kikwete akimjulia hali Hashim Mbita wakati wa uhai wake.
Huwezi kusikiliza tena

Hashim Mbita aaga dunia

Aliyekuwa Katibu Mtendaji wa Kamati ya Ukombozi ya uliokuwa Umoja wa Nchi Huru za Afrika (OAU) kuanzia mwaka 1974 hadi 1994 baada ya Afrika Kusini kupata uhuru, Brigedia Jenerali Hashim Mbita ameaga dunia mwishoni mwa wiki jijini Dar es salaam Tanzania akiwa na umri wa miaka 74.

Nchi za kiafrika hususani zile zilizopata uhuru kupitia katika mapambano ya kijeshi zitamkumbuka kwa namna alivyosaidia kuondoa utawala wa kikoloni katika eneo kubwa la bara la afrika.Kuhusu maisha ya Brigedia Jenerali Hashim Mbita ,Mwanahabari wetu Arnold Kayanda amezungumza na baadhi ya waliopata kuwa karibu na marehemu.