Tetemeko jingine lakumba mji wa Nepal

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Tetemeko jingine lapiga mji wa Nepal

Kumeripotiwa tetemeko jingine lenye nguvu nchini Nepal siku moja baada ya tetemeko kubwa lililosabaisha vifo vya karibu watu 2000.

Watu walikimbia kwenda maeneo ya wazi kwenye mji mkuu wa Kathmandu wakati kulipotokea tetemeko hilo la vipimo vya 6.7 na kutikisa majengo.

Tetemeko hilo nalo lilisikika kaskazini mwa India na Bangaldesh na kusasababisha maporomoko ya theluji katika mlima wa Everest.

Ndege za misaada , madaktari na watoa misaada kutoka nchi jirani zimeanza kuwasili nchini Nepal.

Ndege kutoka India na China zimetua mjini Kathmandu kusaidia katika jitihada za uokozi.