Australia yaiomba msamaha Indonesia

Image caption raia wa Australia wanaotarajiwa kunyongwa kwa kupatikana na hatia ya kufanya biashara ya mihadarati

Waziri mkuu wa Australia Tony Abbot amesema amemuandikia barua rais wa Indonesia Joko Widodo akimuomba awasamehe raia wawili wa Australia ambao walipatikana na hatia ya kuendesha biashara ya dawa za kulevya. Awali rais Widodo alikataa kuzungumza na bwana Abbot kwa njia ya simu.

Waustralia hao wawili wamejulishwa kuwa watauawa ifikapo kesho Jumanne.

Wafungwa hao wawili walihukumiwa mwaka 2006 kwa kuongoza kundi moja lililojaribu kusafirisha dawa aina ya heroin kutoka nchini Indonesia.

Watu hao hao wawili ni miongoni mwa raia wa kigeni waliohukumiwa kifo na ambao wamejulishwa kuwa hukumu zao zitatekelezwa siku chache zinazokuja.

Naye rais wa Ufilipino, Benigno Aquino amemuomba rais Widodo kumpa msamaha mwanamke raia wa nchi hiyo Mary Jane Veloso ambaye ni mmoja wa wanaosubiri kuuawa.