Nahodha: Kifungo cha maisha gerezani

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Lee Jun-Seok , nahodha wa feri ya Sewol.

Mahakama ya rufaa nchini Korea Kusini imempata na hatia ya kuua nahodha wa feri ambayo ilizama mwaka mmoja uliopita na kumuongezea kifungo hadi cha maisha gerezani.

Hukumu hiyo inabatilisha ile ya kwanza ya mahakama ya chini ya mwezi Novemba iliyompata Lee Jun-Seok na hatia ya kuitelekeza meli na kumuhumu kifungo cha miaka thelathini jela.

Jamaa za waathiriwa zililalamikia hukumu ya kwanza zikiitaja kuwa nyepesi.

Zaidi ya watu 300 wengi wao watoto walikufa wakati feri ya Sewol ilipozama. Manusura wengine walisema kuwa waliamrishwa kukaa ndani ya feri huku nahodha akiwa kati ya watu wa kwanza waliookolewa.