Mashambulizi yaendelea Ukrain

Haki miliki ya picha EPA
Image caption Waasi nchini Ukrain.

Ukrain inasema kuwa mmoja wa wanajeshi wake ameuawa na wengine 14 kujeruhiwa kwenye mashambulizi mapya yanayoendeshwa na waasi wanaoiunga mkono Urusi mashariki mwa nchi.

Kifo hicho ndicho cha nne baada ya siku kadha na kilitokea karibu na mji unaoshikiliwa na waasi wa Donetsk.

Serikali inawalaumu waasi kwa kutumia makombora na silaha zingine nzito zilizopigwa marufuku wakati wa makubaliano ya kusitisha vita.

Makubaliano hayo yalistahili kuwa nchini ya uangalizi wa idara ya usalama ya muungano wa ulaya lakini waasi wameizuia idara hiyo kuzuru eneo ambalo inasema kuwa ina silaha nzito.