Tuhuma za ngono Ufaransa zachunguzwa

Image caption Mtuhumiwa wa dhulma ya kingono nchini Ufaransa akiwa katika gari ya polisi.

Waendesha mashtaka nchini Ufaransa wanachunguza tuhuma za ngono kwa watoto zinazodaiwa kufanywa na wanajeshi wa nchi hiyo pindi walipokuwa katika Jamhuri ya Afrika ya Kati.

Wizara ya Ulinzi imesema itahitaji kutolewa kwa adhabu kali zaidi dhidi ya yeyote atakae patikana na hatia.Mashtaka hayo yamefunguliwa baada ya kupatikana kwa nyaraka zilizotolewa mwezi July na mfanyakazi mwandamizi wa Umoja wa Mataifa.

Afisa huyo alisimamishwa kazi baada ya kupeana nyaraka hizo za siri kwa Ufaransa. Farhan Haq, msemaji msaidizi wa katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban ki Moon, amesema Umoja wa Mataifa umefanya uchunguzi wa tuhuma hizo, ambazo itazifuatilia kwa kina.

Nakubaliana na wewe, kwamba jambo lolote linalohusiana na utumikishaji wa ngono na udhalilishaji wa ngono ni jambo la kutiliwa maanani sana. Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa anataka jambo hili lipewe umuhimu wake na mfumo mzima wa Umoja wa Mataifa unataka lishughulikiwe. Katika hili mathalan, ofisi yetu inayoshughulikia maswala ya haki za binadamu imekuwa ikiliangalia hili na kutaka watu wafanyie tathmini. Kwa hiyo, tunataka pia hili lifuatiliwe.)

Farhan Haq amethibitisha kwamba, ingawa tuhuma hizi hazielekezwi kwa walinda amani wa Umoja wa Mataifa, udhalilishaji wa ngono unaofanywa na wanajeshi wanaofanya kazi na Umoja wa Mataifa ni tatizo.

"hili ni tatizo na ni tatizo ambalo tunataka lipatiwe utatuzi, ingawa hivi ni vikosi vyengine, kikosi cha Sangari ambacho kiko chini ya Ufaransa na sio sehemu ya Umoja wa Mataifa. Haijalishi ni nani aliyefanya, bado ni tatizo kubwa, hatutaki watoto wasiokuwa na hatia katika mazingira ya vita kutumiwa vibaya kwa njia hiyo, na inahitaji dhamira, inahitaji kuchunguzwa na iwapo itadhihirika kuwepo kwa makosa, basi sharti mashtaka yafunguliwe.")