Indonesia yawanyonga walanguzi

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Moja ya majeneza yaliyotumiwa kubeba maiti za walanguzi

Indonesia imewanyonga walanguzi wanane wa mihadarati baada ya kutoa hukumu ya kifo dhidi yao.

Hukumu hiyo imetekelezwa na kikosi maalum cha kuwapiga wafungwa risasi, licha ya mwito kutoka kwa mataifa ya dunia ya kuwahurumia watu hao.

Kuuwawa kwa mfungwa wa tisa, raia wa Ufilipino, Mary Jane Veloso, kumecheleweshwa baada ya mwanamke mmoja kujiwasilisha kwa polisi Nchini Ufilipino, akisema kuwa ndiye aliyemhadaa mfungwa huyo mwanamke mwenzake, kupeleka dawa za kulevya hadi Indonesia.

Australia imuita balozi wake kupikinga kuuawa kwa waustral;ia wawili ambao inasema walikuwa wamebadili tabia katika kipindi cha miaka kumi walikuwa kizuizini.

Brazil nayo imesema kuwa kuuawa raia wake wa pili nchini Indonesia ni kisa kibaya kwenye uhusiano kati ya nchi hizo.