Ajuza aliyedhulumiwa kukutana na Abe

Haki miliki ya picha EPA
Image caption Waziri mkuu wa Japan Shinzo Abe

Mwanammke mmoja wa Korea aliyelazimishwa kuwa mtumwa wa ngono na jeshi la Japan wakati wa vita vikuu ya pili duniani atarajiwa kuhudhuria kikao muhimu wakati Waziri Mkuu wa Japan atakapolihutubia baraza la Congress baadaye leo.

Ajuza huyo wa miaka 86 Lee Yong Soo alishikiliwa katika kambi ya jeshi wakati alipokuwa msichana wa miaka 16 na kulazimishwa kutumika kuwaburudisha kingono wanajeshi wa Japan.

Aliyefanikisha mwaliko huo wa Lee Yong Soo huko mjini Washington ni mbunge wa chama cha Democratic, Mike Honda. Mbunge huyo amemtaka Waziri Mkuu Shizo Abe kutumia fursa hiyo leo kuomba radhi kwa maelfu ya wanawake waliodhulumiwa kingono na wanajeshi wa Japan wakati huo wa vita vikuu vya dunia.