Ndege bila rubani zatumiwa Nepal

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Ndege isiyo na ribani au (Drone)

Ndege ndogo zisizokuwa na rubani zinazofahamika kama (Drones) zinatumiwa kusambaza misaada nchini Nepal.

Nchi hiyo ilikumbwa na tetemeko kubwa la ardhi la vipimo vya 7.8 wiki iliyopita ambapo watu wengi waliuawa na uharibifu mkubwa ulitokea.

Shirika la kutoa misaada la Charity Global Medic, linatumia ndege hizo kupiga picha ili kutambua sehemu zilizoathiriwa na tetemeko hilo.

Kisha ndege hizo hutuma picha kwa makundi ya watoa misaada na ya waokoaji walio ardhini.