Faure Gnassingbé ashinda urais Togo

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Rais wa Togo Faure Gnassingbe

Tume ya uchaguzi nchini Togo, imetangaza kuwa Rais, Faure Gnassingbé, ameshinda tena kiti cha urais kwa muhula wa tatu.

Matokeo ya awali yanaonyesha kuwa Rais huyo aliyeingia uongozini mnamo mwaka 2005 amepata zaidi ya asilimia 58 ya kura.

Idadi iliyojitokeza kupiga kura siku ya Jumamosi ilifikia asilimia 60.

Bwana Gnassingbé amekuwa uongozini tangu kifo cha babake, Gnassingbé Eyadema, aliyechukua uongozi wa Togo kwa njia ya mapinduzi mwaka 1967.

Mwaka jana, kulikuwa na maandamano makubwa nchini Togo, huku waandamanaji wakiitaka serikali kubuni sheria ya mihula miwili ya Urais.