Anglikana kukabiliana na hewa ya Carbon

Image caption Askofu mkuu wa kanisa la kianglikana Justin Welby

Kanisa la Kianglikana nchini Uingereza linauza kampuni zake za uwekezaji zinazohusika na kuchimba makaa, na changarawe kama hatua ya kuunga mkono juhudi za kupunguza viwango vya hewa mkaa.

Kasisi Nick Holtham msemaji wa masuala ya mazingira katika kanisa hilo amesema suala la mabadiliko ya tabia nchi linafaa kujadiliwa na pande zote duniani.

Hatua ya kanisa hilo itaathiri uwekezaji wake wa kima cha dola milioni 18.

Kanisa la Kiangilikana ya Uingereza lina uwekezaji wa dola bilioni 12.