Matumaini ya manusura yadidimia Nepal

Image caption Shughuli za kutafuta manusura Nepal.

Matumaini yanadidimia nchini Napal ya kuwapata manusura zaidi baada ya kutokea kwa tetemeko baya la ardhi wiki moja iliyopita .

Msemaji wa wizara ya ndani ya nchi hiyo (Laxmi Prasad Dhakal) alisema, anafikiri kuwa hakuna uwezekano wa kupata manusura zaidi waliofukiwa chini ya vifusi.

Alisema kuwa idadi ya waliokufa sasa imezidi watu 6,600. Maelfu ya watu bado hawajulikani waliko wakiwemo raia zaidi ya 1000 kutoka nchi za ulaya.

Takriban helkopta ishirini zinashiriki katika jitihada za uokoaji katika vijiji vya mbali maeno yaliyo kaskazini mwa nchi.