Shambulizi la muungano lawaua 50 Syria

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Shambulizi la muungano unaoongozwa na Marekani lawaua watu 50 Syria

Ripoti kutoka kaskazini mwa Syria zinasema kuwa zaidi ya raia 50 wameuawa kwenye shambulizi la angani lililoendeshwa na muungano unaongozwa na Marekani.

Shirika la haki za binadamu lenye makao yake nchini Uingereza linasema kuwa kijiji kinachofahamika kama Birmahle kilishambuliwa na kuwa bado watu wamekwama kwenye vifusi.

Muungano huo unaoongozwa na Marekani haujatoa tamko lolote kuhusu kisa hicho kufikia sasa.