Malkia Elizabeth apata kitukuu chengine

Haki miliki ya picha PA
Image caption Mwanamfalme wa Uingereza William apata mtoto wa pili

Mke wa mrithi wa ufalme wa Uingereza Prince William amejifungua mtoto wa kike.

Habari iliyotumwa kupitia kwa mtandao wa Twitter kutoka kwa ikulu ya Kensington ilisema kuwa mtoto huyo alizaliwa akiwa salama kalba ya saa mbili unusu saa za uingeeza.

Mtoto huyo aliye na uzito wa kilo tatu nukta saba alizaliwa muda mfupi baada ya kuwasili kweny hospitali moja mjini London.