Jeshi kutopendelea pande pinzani Burundi

Haki miliki ya picha AP
Image caption Burundi

Jeshi nchini Burundi linasema kuwa litaendelea kuwa na msimamo wa wastani baada ya siku sita za maandamano dhidi ya rais Pierre Nkurunziza.

Waziri wa ulinzi (Pontien Gaciyubwenge) alisema kuwa jeshi ni lazima liheshimu katiba pamoja na makubaliano ya amani yaliyomaliza vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini humo.

Waandamanaji hao wanamlaumu rais kwa kukiuka katiba na makubaliano hayo ya amani kwa kuwania urais kwa muhula wa tatu

Mapema waandamanaji walitangaza kusitisha maandamano kwa siku mbili wakisema kuwa familia zinahitaji muda wa kuwomboleza wale waliouawa kwenye maandamano hayo.