Wafungwa wazusha mapigano,Ugiriki

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Polisi wa kutuliza ghasia,Ugiriki

Takribani wafungwa wawili wamekufa na wengine zaidi ya 20 kujeruhiwa katika mapigano yaliyozuka katika gereza mjini Athens,Ugiriki.

Mamlaka za kisheria nchini humo zinasema kuwa machafuko hayo yalizuka kati ya makundi ya wafungwa raia wa Alabania na Pakistani. Wafungwa hao walitumia baadhi ya vitu katika maeneo yao kama silaha wakati wa mapambano hayo. Hata hivyo haijajulikana mara moja kwamba ni nini hasa kilichosababisha mapigano hayo ya wafungwa.