Al Shabaa wenye nasaba na Al Qaida,wanadhibiti maeneo kadhaa ya Kusini mwa Somalia
Huwezi kusikiliza tena

Al Shabaab wafurahia kuitwa Ugus

Utawala nchini Somalia umeviamrisha vyombo vya habari nchini humo kulipa kundi la wanagamabo wa Al Shaabab jina mpya.

Serikali ya Somalia itaka Al Shaabab kupewa jina la kundi linalowaua watu wa Somalia.

Mkuu wa kitengo cha kitaifa cha ujasusi nchini Somalia (Abdirahman Mohamud Tur-yare) anasema kuwa jina Al Shabab ambalo humaanisha vijana, haliwezi kuhusishwa na wanamgambo.

Hata hivyo hakuna tamko lolote lililotolewa kama adhabu kwa yeyote atakaye kiuka agizo hilo .Serikali ina miliki vyombo vya habari kama Radio Mogadishu na runinga ya SNTV na vyombo hivyo vimekuwa vikilitumia jina hilo la Ugus muda mrefu uliopita.

Vita vya kisiasa kati ya pande hizo mbili kati ya serikali ya Somalia na kundi hilo la al-Shabab vimekuwepo tangu mwaka 2009, wakati ambapo al-Shabab walipotangaza vita na raisi wa serikali ya shirikisho , Sheikh Sharif Sheikh Ahmed. Tangu wakati huo ,pande mbili hizo zimekuwa zikibadilishana ujumbe wa vijembe baina yao katika vyombo vya habari .

Waandishi habari nchini Somalia kwa sasa wako njia panda,wanapaswa kuwa na uchaguzi wa kutii agizo hilo ama wakumbane na hasira ya kundi hilo la al-Shabab, ama waamue kukaidi agizo la serikali na wakabiliane na matokeo ya ukaidi wao. Siku za hivi karibuni serikali ya Somalia imekwisha wakamata waandishi habari na kuzifungia redio kadhaa kwa madai ya kuhatarisha usalama wa taifa hilo.

Ifuatayo ni taarifa ya mwandishi wa BBC, aliyeko Nairobi, abdulahi abdi na kwanza anafafanua maana ya jina hilo Ugus.