Saa za Apple zakosolewa

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Saa za Apple aina ya Smart watch

Kampuni ya Apple imekiri kwamba 'tattoo' za kifundo cha mkononi zinaweza kuathiri uangalizi wa moyo wa binaadamu katika saa za kampuni hiyo ,siku chache tu baada ya malalamishi kutoka kwa watu walio na 'tatoo' kwamba saa hizo aina ya Smartwatch haziweza kusema iwapo wako hai ama la.

Tatizo hilo limezuka kwa sababu saa hiyo hutumia miale ya rangi ya kijani inayong'ara ndani ya ngozi ili kubaini kiwango cha moyo unavyopiga.

Lakini kwa watu walio na 'tattoo' katika kifundo cha mkono ,wino unaotumika huzuia mwangaza huo wa kijani kibichi na hivyobasi kutoa matokeo mabaya.

Image caption saa za Apple

Kampuni ya Apple hatahivyo haijatoa tamko lolote kuhusu habari hiyo lakini imearifu ukurasa wa usaidizi wa saa hiyo kubaini tatizo hilo.

Huku kampuni hiyo ikiwa imeliangazia swala la kiwango cha moyo wa binadaamu unavyopiga,na kusahau kwamba wateja wake wamekuwa wakilalamika kuhusu sensa ya ngozi katika saa hiyo,ambayo inachukua habari za iwapo saa hiyo imevuliwa na inawabidi watumiaji kuweka neno la siri.