Watu 3 wauawa katika maandamano Burundi

Image caption Ghasia Burundi

Takriban watu wawili wameuawa wakati wa ghasia kati ya polisi na waandamanaji kwenye mji mkuu wa Burundi Bujumbura .

Polisi walifyatua risasi huku waandamanaji wakirusha mawe na guruneti.

Image caption Ghasia Burundi

Polisi wawili na waandamanaji sita nao walijeruhiwa.

Waandamanaji hao wanalalamikia hatua ya rais Pierre Nkurunziza ya kuwania urais kwa muhula wa tatu.