Hamkani si shwari Burundi
Huwezi kusikiliza tena

Rais Kikwete atuma ujumbe nchini Burundi

Takriban watu watatu wameuawa wakati wa ghasia kati ya polisi na waandamaji kwenye mji mkuu wa Burundi Bujumbura .

Polisi walifyatua risasi huku waandamajii wakirusha mawe na guruneti.

Waandamanaji hao wanalalamikia hatua ya rais Pierre Nkurunzinaza ya kuwania urais kwa muhula wa tatu.

Kufuatia sintofahamu hiyo mwandishi wetu Regina Mziwanda amezungumza na Mindi Kasiga mkuu wa kitengo cha mawasiliano ya serikali kwa umma kutoka mjini Dar-Es-Salaam anafafanua juu ya ujumbe unaotumwa na rais Kikwete kama mwenyekiti wa EAC nchini Burundi .