Apata umaarufu kwa kupiga picha na sodo

Image caption Sodo

Kijana mmoja nchini Marekani amesifiwa kwa kugawa picha yake ya 'selfie' {ya yeye mwenyewe} akibeba sodo huku akiwataka vijana wenzake kumuiga ili kuwasadia wasichana iwapo watapatikana katika hedhi na hawana sodo.

Kijana huyo wa miaka 15 Jose Garcia ambaye ana wafuasi 16,000 amewapatia changamoto vijana wenzake kubeba sodo wakati wanapoenda shule ili kuwasaidia wasichana.

Amesema kuwa licha ya kuwa wavulana hawajali kuhusu swala la hedhi ,ni muhimu kujua kwamba hedhi inaweza kumpata msichana bila kujua na kuwa vigumu kwa yeye kupata sodo.

Neno #realmensupportwomen limependwa na zaidi ya watu 20,000.