Mike Tyson hapendi picha binafsi

Image caption Mike Tyson akimng'akia shabiki aliyeamua kujichukulia picha binafsi bila taarifa.

Mashabiki wa mwanamasumbwi nguli wa kitambo Mike Tyson wana tatizo moja kubwa,ni namna gani wanaweza kujipiga picha pamoja naye? Na hata ukipata bahati ya kupiga picha pamoja naye uhakikishe hutamuudhi, ni jambo ambalo halitabiriki.

Mmoja wa watu wanaomfakilia Mike Tyson,aliamua kubwia funda kadhaa za pombe ili auvae ujasiri na aijaribu bahati yake na kumkaribia mkali huyo wa ulingo ili apate picha binafsi, lakini bahati haikuwa yake.

Tukio hili halikutokea kitambo ni juzi kati tu wakati wa pambano kubwa lililoukamata ulimwengu na kuwa na kiu inayofanana ya kushuhudia nani mbabe kati ya Floyd Mayweather na Manny Pacquiao na hatimaye tajiri Mayweather ambae jina lake la utani ni Money, alipokea zaidi ya dolla millioni $150m na Pacquiao kuambulia millioni $100m.,video hiyo ilinaswa kwenye picha za video na kuzunguuka dunia na inamuonesha Tyson akiwa katika taharuki na kung’aka kufuatia kuchukuliwa poa .

Mwanamasumbwi huyo nguli wa zamani ulingoni ambaye sasa ana miaka arobaini na nane ambaye kwa hiari yake aliamua kustaafu kuvurumisha ngumi zenye uzito wa kilo mia mbili,alionekana akigeuza shingo yake kwa mshangao ,wakati shabiki wake alipokuwa katika harakati za kujipiga picha huku akihakikisha mkali huyo yumo kwenye picha hiyo,na kabla shabiki huyo hajazidi kumkera na kuonekana sugu kuelewa vitendo vya Tyson kuwa anakereka kwa vitendo vyake.

Pamoja na mkali huyo kumuashiria kumpotezea naye kutotaka kuonekana kwenye picha hiyo,Tyson sasa akaanza kurusha kiwiko chake cha mkono ili kumlazimisha shabiki wake huyo kuachana na jaribio hilo

Ingawa kwa kuvurumisha kiwiko hicho hakukuwa kwa lengo la kumdhuru shabiki huyo ,lakini kutokana na ubavu wake ‘Iron Mike’ilikuwa wazi kabisa shabiki huyo kusukumwa kwa nyuma na watu walioelewa asichokitaka mkali huyo wa ulingo.

Ni wazi hii inadhihirisha wazi kuwa usithubutu kumkaribia nguli huyo wa masumbumbwi maana lolote laweza kutokea.