IS yakiri kutekeleza shambulizi Texas

Haki miliki ya picha REUTERS
Image caption Shambulizi la Texas

Wapiganaji wa kundi la Islamic State wamekiri kwamba ndio waliotekeleza shambulizi katika shindano la vibonzo vya kumkejeli mtume Muhammad (s.a.w.) katika jimbo la Texas nchini Marekani.

Kundi hilo limesema kuwa wapiganaji wawili wa kundi hilo walitekeleza shambulizi hilo katika mkutano uliokuwa karibu na mji wa Dallas.

Taarifa ya habari ya Redio ya kundi hilo Al-Bayan imesema kuwa maonyesho hayo yalikuwa yakionyesha picha mbaya kumhusu mtume Muhammad.

Washukiwa wote wawili walipigwa risasi baada ya kufyatua risasi katika maonyesho hayo siku ya jumapili.