Milipuko yatokea jeshini Sudan

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Rais wa Sudan Omar Al Bashir

Kumetokea milipuko katika maeno ya jeshi nje ya mji mkuu wa Sudan, Khartoum.

Wakazi katika wa eneo la Omdurman la ukanda wa magharibi wa mto Nile wamesema mapema usiku wa manane walisikia mlipuko wa kwanza na baadae makombora ya kutungulia ndege kutoka upande wa majeshi ya serikali.

Msemaji wa serikali ya Sudan amethibitisha askari wake walifanya mashambulizi na kulenga kundi wasilolifahamu lakini akakanusha kikosi chake na vifaa vyao vya kijeshi kushambuliwa.

Miaka mitatu iliyopita Sudan iilituhumu Israeli kwa kufanya mashambulizi ya anga kwenye kiwanda cha silaha mjini Khartoum ambapo pia kuna taarifa kuwa ndege za Israel pia zilifanya mashambulizi kwenye misafara ya silaha zilizokuwa zikisafirishwa kwenda Gaza.

Israel haijatoa taarifa zozote rasmi kujibu shutuma hizo.