Aliyetoa siri ya ngono CAR kurudi kazini

Haki miliki ya picha un.org
Image caption Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon

Mahakama ya Nidhamu ya Umoja wa Mataifa imetoa hukumu ya kwamba adhabu ya kusimamishwa kazi kwa Afisa wa ngazi ya juu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Haki za Binadamu kwa kosa la kutoa taarifa iondolowe mara moja.

Afisa huyo Anders Kompass, alitoa taarifa kwa mamlaka za Ufaransa kwamba majeshi ya Ufaransa ya kulinda ya amani huko Jamuhuri ya Afrika ya Kati walihusika kuwanajisi watoto.

Ataruhusiwa kurudi kazini mara baada ya shauri lake kupitiwa na maafisa wa ndani ya shirika hilo.

Umoja wa mataifa umekanusha kutaka kufunika tuhuma hizo.