Taleban yalazimu jeshi kulinda mji wa Kunduz

Haki miliki ya picha AP
Image caption Taleban yalazimu jeshi kulinda mji wa Kunduz Afghanistan

Wajeshi wa Afghanistan wametangaza kuwa, wamewauwa zaidi ya wapiganaji 35 wa Taliban katika makabiliano makali waliyoianzisha leo.

Makabiliano hayo yalilenga mji wa Kunduz, Kaskazini mashariki mwa Nchi hiyo.

Taarifa rasmi ya serikali ya Aghanistan inasema kuwa, vijiji kadhaa vilivyokuwa vikikaliwa na Taliban vimerejeshwa upande wa serikali.

Mwaandishi habari wa BBC mjini Kunduz, anasema kuwa mapigano yamekuwa yakiendelea kilomita kadhaa kutoka mji huo, na kwamba anasikia milio ya mizinga.

Inakisiwa kuwa, zaidi ya watu laki moja wameathirika na mzozo huo.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Majeshi ya Afghanistan yakishika doria

Gavana wa jimbo hilo Mohammed Omer Safi, amesema kuwa, wapiganaji wa jihadi wa Islamic State, wanapigana kwa pamoja na Taliban, huku wakiwaunga mkono.

Mwaandishi wa BBC aliyeko huko anasema kuwa majeshi ya Afghanistan, yanakosa mitambo ya kisasa ya mawasiliano,na amewaona makamanda wa vikosi vya serikali, wakitumia simu zao za rununu kuwasiliana na makao makuu Mjini Kabul.