Barcelona yaidhalilisha Bayern 3-0 UEFA

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Lionel Messi wa Barcelona

Lionel Messi amefunga mara mbili katika pambano kali la nusu fainali za pili za kombe la mabingwa barani Ulaya, zikiwa zimebakia dakika 13 mchezo kumalizika dhidi ya timu machachari ya Bayern Munich.

Wenyeji walionekana kujitayarisha kukabiliana na hali ya kuchanganya kabla ya Messi kubadili mwelekeo huo na kuwa furaha.

Dakika tatu baadaye Messi aliiadhibu Bayern baada ya kumpita mlinzi Jerome Boateng na kufunga kilaini.

Kikosi cha Bayern kikiongozwa na kocha wa zamani wa Barcelona Pep Guardiola, kilizidisha mashambulizi japo kupata bao la ugenini, matokeo yake ni kuadhibiwa tena na Neymar katika dakika ya 90

Hadi kufikia matokeo hayo ya kuchanganya, Bayern walionyesha uwezo mkubwa wa kusakata soka.

Barcelona na Bayern zitarudiana tarehe 12 Mei katika uwanja wake wa Allianz Arena, Ujerumani.