Uingereza 2015:Ashinda dau la £210,000

Haki miliki ya picha AP
Image caption Uingereza 2015:Ashinda dau la £210,000 baada ya Conservatives kupata ushindi mkubwa

Mwanaume mmoja mwenyeji wa Glasgow Scotland aliyebashiri ushindi mkubwa wa The Conservatives sasa ameibuka mshindi wa dau la dola laki tatu .

Bwana huyo mkaazi wa Ladbrokes aliweka dau la pauni elfu thelathini (£30,000) akibashiri ushindi wa the Conservatives siku 10 zilizopita.

Wakati huo watatu wachache mno walikuwa wakiipigia upatu chama cha Conservatives kupata ushindi.

Mwanaume huyo alikuwa wa pekee kati ya wengine saba aliyewekea dau akiipigia upatu Conservatives na sasa ndiye aliyeibuka mshindi mkubwa wa pauni laki mbili £210,000.

Afisa mmoja wa kampuni ya Ladbrokes Alex Donohue alisema ''Mwanaume huyo aliyekuwa amevalia nadhifu mno na mchache wa maneno ndiye mshindi mkubwa katika uchaguzi wa mkuu''.

Bwana Donohue amesema watu wengi sawa na wenye mashirika ya kutoa kura za maoni walikuwa wamebashiri kuwepo kwa serikali ya muungano lakini wapi

Image caption Ushindi wa Conservative wampa kipato cha pauni laki mbili

Wapiga kura walikuwa na mawazo tofauti.

Waziri mkuu David Cameron amepata ushindi mkubwa katika uchaguzi mkuu uliofanyika nchini Uingereza hiyo jana.

Chama chake cha Conservative kimejipatia kura 330

Chama kikuu cha upinzani Leba kimesajili jumla ya viti 232 hii ikiwa na viti 26 chini ya idadi iliyokuwa nayo katika bunge lililopita.

Wakati huohuo habari zinazotufikia ni kwamba Nick Clegg amejiuzulu kama kiongozi wa chama cha Liberal Democrat baada ya kushindwa na chama cha Conservative