wakimbizi wa Burundi wakisubiri majaaliwa ya kuingia Tanzania
Huwezi kusikiliza tena

Raia wa Burundi waomba hifadhi Tanzania

Zaidi ya raia elfu 20 kutoka mkoa wa makamba na Ruminge nchini Burundi wapo katika eneo la Kagunga mkoani Kigoma magharibi mwa Tanzania wakitaka kuvuka ziwa Tanganyika na kuingia nchini Tanzania kwaajili ya kuomba hifadhi.

Shirika la kuhudumia wakimbizi ulimwenguni UNHCR Tayari limekodi meli kongwe ya mv Liemba kuwasafirisha raia hao kwenda katika makambi ya wakimbizi ya mkoani Kigoma.

Mwandishi wa BBC Leonard Mubali amesafiri na Meli hiyo hadi katika eneo hilo na kutuandalia taarifa ifuatayo.