Ufisadi: Mawaziri wote kujiuzulu Chile

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Rais wa Chile Michelle Bachelet amelitaka baraza lake lote la mawaziri kujiuzulu.

Rais wa Chile Michelle Bachelet amelitaka baraza lake lote la mawaziri kujiuzulu.

Rais Bachelet amechukua hatua hiyo kufuatia misururu ya kashfa za kisiasa ambazo zimesababisa umaarufu wake kudidimia.

Rais amesema kuwa ataamua ndani ya saa 72 kuhusu ni nani atakubali ajiuzulu na yule atakataa.

Bi Bachelet aliingia madarakani mwaka uliopita kufuatia ushindi mkubwa lakini umaarufu wake umetatizwa na kashfa za ufisadi zinazomwandama mwanawe wa kiume.

Mwanawe wa kiume alijiuzulu mwezi Februari kufuatia kashfa ya kutumia ushawishi .

''Muda mchache uliopita nilitoa agizo kwa serikali yote kujiuzulu lakini katika kipindi cha chini ya saa 72 nitatoa mwelekezo wa yupi anayebaki na yupi atang'atuka.

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Mwanawe wa kiume alijiuzulu mwezi Februari kufuatia kashfa ya kutumia ushawishi wake mbaya .

''Nafikiri muda umewadia kwa mabadiliko ya kimsingi kufanyika'' alisema rais.

Mwanawe bi Bachelet , Sebastian Davalos,alituhumiwa ka kutumia ushawishi wake kumpa mkewe mkopo wa dola milioni kumi $10m.

Bi Bachelet, ni mwanamke wa kwanza na rais wa kwanza kuwahi kuwafurahisha zaidi ya asilimia 80 ya watu nchini Chile alipoingoza taifa hilo kati ya mwaka wa 2006 na 2010 .

Lakini aliporejea kwa awamu ya sasa kura za maoni zimekuwa zikimpa takriban thuluthi moja ya ushawishi nchini humo.