Netanyahu aunda serikali ya umoja Israel

Haki miliki ya picha EPA
Image caption Waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu

Waziri mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu, amefikia mkataba wa kuunda serikali mpya ya pamoja, muda mfupi kabla ya kumalizika kwa muda uliokuwa umepangwa.

Makubaliano yake na chama cha mrengo wa kulia cha Kiyahudi, Jewish Home Party yanamhakikishia kupata wingi wa wabunge katika bunge la Israel, japo kwa kiasi kidogo akiwa na viti 61 katika bunge la wajumbe 120.

Chama hicho cha Kiyahudi kinachotetea upanuzi wa makazi ya Wayahudi katika maeneo ya Wapalestina, kimepewa wizara muhimu ya Sheria. Muungano huo pia unakihusisha chama cha ultra Orthodox.

Katika mkutano wa waandishi wa habari, ukihudhuriwa na kiongozi wa chama cha Kiyahudi, Naftali Bennett, Bwana Netanyahu amesema kazi kubwa katika kuunda serikali ya pamoja.

Chama cha Bwana Netanyahu cha Likud kilishinda uchaguzi wa mwezi Marchi kwa kupata viti 30.