Nkurunziza awasilisha stakhabadhi za urais

Image caption Rais wa Burundi akiwasilisha stakhabadhi zake kwa tume ya uchaguzi

Rais wa Burundi, Pierre Nkurunziza, amewasilisha rasmi stakabadhi zake za kuwania kiti cha Urais, kwa tume ya uchaguzi mkuu mjini Bujumbura.

Upinzani unasema kuwa, muhula wa tatu wa Urais unakiuka katiba ya nchi hiyo.

Mapema juma hili mahakama nchini Burundi ilimuidhinisha Nkuruzinza kuwania tena kiti hicho kwa muhula wa tatu.

Upinzani unasema kuwa waandamanaji 17 wameuawa katika ghasia zilizodumu majuma mawili nchini humo kupinga uamuzi huo wa Rais.