Aspirin na Ibuprofen hupunguza saratani

Image caption saratani ya utumbo mkubwa wa binaadamu

Utumizi wa aspirin na Ibuprofen unapunguza hatari ya kushikwa na saratani ya utumbo lakini hazifanyi kazi katika idadi ndogo ya watu walio na jini tofauti,watafiti wanasema.

Utafiti huo uliofanywa na jarida la muungano wa matibabu nchini Marekani JAMA unatokana na uchanganuzi wa tafiti 10 nchini Australia,Canada,Ujerumani na Marekani.

Zaidi ya watu 16,000 wote wakitoka Ulaya walishirikisha.

Data iliopatikana ilithibitisha kwamba utumizi wa mara kwa mara wa dawa ya aspirin unahusishwa na kushuka kwa viwango vya ugonjwa wa saratani unaohusishwa na utumbo kwa asilimia 30.