Mali ya Aboutrika yazuiliwa Misri

Haki miliki ya picha BBC World Service
Image caption Mohammed Aboutrika

Mamlaka nchini Misri imechukua Mali ya aliyekuwa mchezaji nyota wa taifa hilo Mohammed Aboutrika kufuatia madai kwamba alihusika kulifadhili kundi lililopigwa marufuku nchini humo Muslim Brotherhood.

Akijibu hatua hiyo Aboutrika amesema kuwa hatolitoroka taifa hilo na kwamba ataendelea kuhakikisha kuwa kuna ufanisi nchini humo.

Mchezaji huyo ambaye aliwahi kuwa mmoja ya nyota wa soka barani Afrika alimuunga mkono hadharani rais aliyeng'atuliwa mamlakani Mohammed Morsi wakati alipowania urais mwaka 2012.

Serikali ya rais Abdel Fattah al Sisi ambaye alimuondoa madarakani Mohammed Morsi imekuwa ikiwasaka wanachama wa kundi hilo.