Liberia kutangazwa taifa lisilo na Ebola

Haki miliki ya picha
Image caption Mgonjwa wa mwisho wa Ebola nchini Liberia

Shirika la afya duniani WHO linatarajiwa kuitangaza Liberia kuwa isiyo na ugonjwa wa ebola wakati litakapothibitisha kuwa nchi hiyo haina kisa chengine kipya kwa siku 42 zilizopita.

Rais wa Liberia Ellen Johnson Sirlieaf anasema kwa Liberia sasa itasherehekea jitihada zake za kupambana na ugonjwa huo.

Liberia iliripoti kisa chake cha kwanza zaidi ya mwaka mmoja uliopita wakati ugonjwa huo uliposambaa kutoka taifa jirani la Guinea.

Ugonjwa huo umewaua zaidi ya watu 11,000 katika eneo la Afrika magharibi.