Wafungwa,na walinzi wauawa katika jela Iraq

Image caption Jela ya Iraq

Askari polisi kadhaa wa Iraq pamoja na wafungwa karibia 30, wameuawa, wakati wafungwa zaidi ya 50 walipotoroka jela moja kaskazini mashariki mwa Baghdad.

Duru za polisi zinasema ghasia hizo zilianza katika gereza la Al-Khalis, pale wafungwa walipoanza kupigana.

Walinzi waliingilia kati, lakini walishambuliwa na kuzidiwa nguvu, kabla ya kunyan'ganywa silaha, na wafungwa wakaanza kutoroka.

Lakini duru za eneo hilo zinasema kuwa wafungwa walitoroka baada ya wapiganaji wa Islamic State kushambulia gereza, kujaribu kuwatoa wenzao waliokuwemo .