Mubarak na wanawe wafungwa miaka 3 Misri

Haki miliki ya picha AP
Image caption Hosni Mubarak na wanawe wawili wamehukumiwa kifungo cha miaka mitatu jela

Mahakama ya uhalifu ya Misri imetoa hukumu ya kifungo cha miaka mitatu, kwa rais wa zamani, Hosni Mubarak, na watoto wake wawili wa kiume,kutokana na kesi ya rushwa iliokuwa ikiwakabili.

Mwaka jana, wote watatu walipatikana na hatia ya kutumia fedha za taifa, kukarabati nyumba za familia yao.

Lakini mahakama ya rufaa ilifuta kesi hiyo na kutaka kesi ifanywe tena.

Bwana Mubarak alipatikana hana makosa, katika kesi zote nyengine, pamoja na kuamrisha mauaji ya waandamanaji, katika mwamko wa Januari mwaka 2011, ambao ulimaliza utawala wake wa miaka 30.

Washtakiwa hao watatu huenda wasitumikie kifungo kwa sababu ya muda waliokaa kizuizini.

(Wana siku 60 kukata rufaa dhidi ya hukumu hiyo.)