Kimbunga Noul kupiga Ufilipino kaskazini

Haki miliki ya picha AP
Image caption KImbunga Noul kinatarajiwa kupiga kazkazini mwa Ufilipino

Wakazi wa maeneo ya kaskazini mwa Ufilipino wanajiandaa kuwasili kwa kimbunga ambacho tayari kimesababisha kufutiliwa mbali kwa safari za ndege na usafiri wa baharini.

Kimbunga hicho kinachojulikana kama Noul kilicho na upepo unaovuma kwa kasi ya zaidi ya kilomita 160 kwa saa, kinatarajiwa kuwasili eneo hilo muda mfupi unaokuja.

Maafisa kwenye mikoa iliyo kaskazini ya Isabela na Cagayan wanasema kuwa wamechukua tahadhari na wako tayari kuwahamisha watu kutoka nyanda za chini.