Mashambulizi zaidi yafanyika Yemen

Haki miliki ya picha AP
Image caption Mashambulizi nchini Yemen

Vikosi vinavyoongozwa na Saudi Arabia vimeendesha mashambulizi kwenye mjii mkuu Yemen sanaa vikilenga nyumba ya rais wa zamani Ali Abdullah Saleh.

Milipuko mikubwa ilisikika na moshi mkubwa ulionekana ukitanda angani kutoka eno hilo. Rais huyo wa zamani ni mshirika wa waasi wa Houthi ambao wanaendesha harakati za kutaka kuidhibiti Yemen.

Hata hivyo haiaminiki ikiwa alikuwa kwenye nyumba hiyo.

Mapema mjumbe wa umoja wa mataifa nchini Yemen (Johannes Van Der Klaauw) alivilamu vikosi vinavoongozwa na Saudi Arabia kwa kufanya mashambulizi ya kiholela nchini humo.

Alionya kuwa kulenga maeneo yenye watu wengi, licha ya kutoa onyo la mapema, ni ukiukaji wa sheria za kimataifa.