Hollande kukutana na Castro wa Cuba

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Holande anatarajiwa kukutana na rais wa Cuba Raul Castro baadaye leo.

Rasi wa Ufaransa Francois Hollande yuko nchini Cuba ikiwa ndiyo ziara ya kwanza kufanywa na rais wa Ufaransa kwa zaidi ya karne moja.

Holande anatarajiwa kukutana na rais wa Cuba Raul Castro baadaye leo.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Hollande anakuwa rais wa kwanza wa Ufaransa aliye madarakani kufika nchini cuba kwa zaidi ya karne moja iliyopita

Akiwasili mjini Havana rais Hollande anakuwa rais wa kwanza wa Ufaransa aliye madarakani kufika nchini cuba kwa zaidi ya karne moja iliyopita.

Lakini pia ndiye afisa wa kimataifa wa cheo cha juu kukizuru kisiwa hicho tangu uhusiano kati ya Cuba na Marekani utangazwe kuboreka mwezi disemba.

Uingereza , Uholanzi, Japan na Urusi tayari wametuma waakilishi wao kwenda Cuba kati miezi ya hivi majuzi.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Hollande anakuwa rais wa kwanza wa Ufaransa aliye madarakani kufika nchini cuba kwa zaidi ya karne moja iliyopita

Kinyume na washirika wake barani ulaya Ufaransa imedumisha uhusiano wake na taifa hilo la kiKomunisti.

Rais Hollande ameandamana na wajumbe wa karibu wafanyibiashara 20 kutoka Ufaransa.